NGUVU KATIKA JINA ULILONALO


JINA LAKO LINA BEBA HATMA YAKO.
Watu Wengi Wamepewa Majina ya Ajabu mara Shida,Taabu wengine Masumbuko ebu jaribu kuangalia Watu wenye Majina Hayo wakoje.Pia unaweza ukapewa jina hilo na mafariki hata watu karibu kutokana na Tabia Yako au Mambo Unayoyafanya kama ni mwizi utapewa majina ya watu ambao waliwahi kuwa waizi kama unatabia za kichangudoa utapewa majina ya watu ambao wanafahamika ni machangudoa.Nakumbuka nilivyo kuwa mdogo wakati naabudu kanisa la Katoliki nilikuwa napenda sana kutumikia ikafika mahali wazazi wangu wakaanza kuniita Padre ,na sikuwaambia waniite hivoo ila wao tu waliona labda mwenendo wangu naweza kuja kuwa Pandre.Na pia nilipokuwa Primary nakumbuka nilikuwa mtundu na mkorofi sana mpaka watoto wenzangu wakaamua kuniita Idd Amini.kadri siku zinapoenda na ninapozidi kukua majina yanabadilika kutokana na Tabia yangu ambayo watu wanaiona kwangu na nilipokuwa O Level nilikuwa napenda sana habari za siasa na nikawa ila nlikuwa sitaki kugombea uongozi wa shule watu wengi wakawa wananiita Obama ila wako wengine pia waliniita mchungaji na mpaka sasa wananiita hivo.



Na hilo jina unalopewa huwa linakukaa vizuri sana mfano umepewa jina la shida hata kama uko vizuri kidogo kidogo unaanza kupata matatizo mpaka jina la shida linakukaa vizuri.Kuna watu wengine wanapewa majina mazuri na marafiki au watu wao wakaribu kwa sababu labda wamefanana na mtu fulani mrembo au handsome bila kuchunguza undani wa yule mtu yukoje.kila jina la mtu unayepewa ambaye nae lina roho ambayo itakufuatilia,kama wewe ni mzuri na umepewa jina baya ile roho itakufuata na kuhakikisha umekuwaa mbaya,inawezekana pia huyo mtu unayefananishwa nae ni mlevi ile roho itakufuatilia mpaka na wewe uwe mlevi.Hakikisha kila jina unalopewa kama ni baya likatae kwa jina la Yesu maana hayo mamlaka tunayo,ila pia kama ni zuri litakase na ukatae hizo roho za mtu mwenye jina hilo zisikufuatilie. muhimu pia kujua watu wakaribu yako wanakuitaje mfano mzuri Yesu aliwauliza wanafunzi wake watu wanasema mimi ni nani ?na baada ya hapo akawauliza na nyie mnasema mimi ni nani ?


Jina Yesu :Tunaona hatma ya jina la Yesu lilimpeleka mpaka msalabani kwa sababu Jina lina maana ya Ukombozi ,kwa hiyo ili atukomboe ilimbidi afe kukamilisha kusudi lake hapa duniani. Kikubwa kwako ndugu msomaji jichunguze je unapewa majina gani kama ni ni kwasababu ya tabia uliyo nayo kataa au kama ni kwasababu ya maisha uliyo nayo au mambo unayopitia kataa hayo majina na ukubali mabadiliko ya kuitwa majina mazuri kwani ndio yanayo kunenea mema.


By Gerald Brown

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment