Kiasubuhi kikaanza na kimvua bana...lakini hakikwamisha chochote,kwa jinsi watu walivyopania yaani wakatembea nacho mdogo mdogo mpaka kituoni....khaaaaaaa kufika si dereva bado hajawasili.
Kuanza kumtafuta tafuta hewani nae akawa anaweka weka kiuongo cha kwenye simu oooh mara nakaribia mara sijui niko TANAPA.........ila bado shauku haikutoka yaani,watu wakasubiri tuuuuu..haikuchukua dakika akafika,basi vimizigo vikapakiwa na watu wakajitoma ndani tayari kwa safari yenyewe.
Masaa mawili tu yalitosha kufikisha watu kwenye hifadhi za Manyara kutokea Arusha town...People were excited baada ya kuona lango lenyewe la kuingilia huku kwa mbali Ngedere wakianza kuwakaribisha.After few minutes taratibu za kujiregister zilikua zimekamilika sasa watu wakapewa ruksa rasmi za kuanza kutalii.
Kulikua na viboko,swala,twiga,nguchiro,nyati,nyumbu,ngiri,ngedere na nyani wa kutoshaaaaaaaa tena walivyofurahi kuwaona CBCG wakawa wanazuia hadi njia watu wasiondoke yaani.
The adventure ilinoga zaidi pale gari ilipokwama....ikabidi kuanz kufanya jitihad za kuipush itoke....tunamshukuru MUNGU kwasababu tulifanikiwa,lakini pia askari wanyama pori kwa msaada mkubwa waliotoa.
Tour ikaendelea...watu wakala msosi wa kushiba na vinywaji vya kushushia pale..halafu muda wa kuongea ukapatikana;watu especially wageni wakaelezwa kuhusu the initiative,wakauliza maswali na majibu yakatolewa.....lakini pia nafasi ikatolewa ya wao kujiunga kwenye mpango huu kabambe ikatolewa na wakafanya hivyo.
Baada ya kumalizia kwenye sehemu ya maji moto,safari ya kurudi Arusha town ikaanza...kumbe mambo hayakuishia tu kwenye hifadhi tu hata kwenye basi vitu viliendelea.
Mafundisho yakaendelea kutolewa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa initiative na watu wengine waliohudhuria....ilikua poa mnooooo,watu walijengwa na kujengeka yaani na utukufu ukamrudia Bwana Mungu wa Majeshi maana sisi sote ni viumbe wake na tunatumiwa tu kama vyombo ili kazi yake iende.
Shukrani ziwaendee uongozi mzima wa CBCG,mabalozi wake wote na watu wote waliofanikisha tour hii ndogo lakini yenye impact kubwa....MUNGU awabariki na karibuni tena mshiriki nasi63
.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment